Na Amiri Kilagalila,Njombe
TAKWIMU za wanachama wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Njombe zinatajwa kuongezeka na kufikia idadi ya wanachama 60,510 kutoka wanachama 58,700 kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 huku ongezeko hilo likitajwa kuwa bado halilidhishi.
Idadi hiyo ya wanachama imetajwa na katibu wa CCM wilaya ya Njombe Hanafi Msabaha katika kikao cha kawada cha sekretarieti ya mkoa wa Njombe na viongozi mbali mbali wa chama hicho halmashauri ya mji wa Makamabako yenye lengo la kukagua uhai wa Chama,miradi ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa maagizo ya chama katika wilaya hiyo.
“Tulikuwa na wanachama 58,700 lakini mpaka jana tunawanachama 60,510 wilaya nzima ya Njombe”alisema Msabaha
Amesema Chama kinaendelea na zoezi la kuhamasisha wengeni kujiunga na chama hicho huku zoezi jingine linaloendelea kwa sasa ni uandikishaji kwa njia ya kielekroniki japo licha ya mfumo huo kuwa na changamoto lakini wamekwisha andikisha wanachama 18,900.
“Mwaka 2019 tulianza zoezi la uandikishaji wanachama kwa mfumo wa kielektroniki na waliandikishwa wanachama 17,000.Lakini mpaka jana tuna wanachama 18 elfu na kama 900 hivi ambao wamekwishaandikishwa kwa mfumo wa kieletroniki,kazi hiyo ni ya kudumu tunaendelea nayo na inachangamoto ya vifaa vya usajili na tumejipanga kupitia kamati za siasa angalau kila kata iwepo simu kwa ajili ya usaili wa wanachama”alisema Msabaha
Kuhusu swala kuanzisha miradi ili kukuza uchumi wa wa chama,Msabaha amesema Chama hicho kimeendelea na zoezi la kuanzisha miradi mipya huku mpaka sasa wakiwa wamefungua mipya 7
“Mpaka wiki ilyopita tumekuwa na miradi mipya 7 ya kiuchumi,miaradi 3 nia ya wilaya na mingine ni ya kata na matawi huku miwili ni jumuiya na tumekubaliana kuhakikisa mpaka mwaka 2024 angalau tuwe tumefikia 50% ya matawi yetu ambayo hayana ofisi tuwe tumejenga ofisi”alisema Msabaha
Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole ametoa wito kwa wanachama wa chama hicho kuendelea kuongeza wanachama kwa nguvu pamoja na kulipa ada zao.
“Sasa nendeni mkalipe ada,tunataka tufanye maajabu kwenye mkoa huu kwasababu tuko nafasi mbaya ya 10 kutoka mikoa ya mwisho inayofanya vibaya Tanzania ili twende tatu bora zinazofanya vizuri tutoke kwenye aibu hii”alisema Ngole
Kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Njombe Amina Imbo,amesema Chama hicho kitaendelea kusimamia utekelezaji wake wa Ilani katika serikali pamoja na kuhakikisha Chama kinakuwa na vyanzo vya mapato ili kiweze kujitegemea.
“Lakaini niwapongeze sana wilaya ya Njombe kwa kuwa inaongoza kwenye mkoa wetu katika swala la vyanzo vya mapato,na ukiangalia hapa sasa mnavuka kwenye wilaya na kenda kwenye kata,na sisi tunataka mfanye makubwa zaidi kitaifa”Alisema Amina Imbo
Akizungumza kwa niaba ya madiwani na viongozi wote waliofika katika kikao hicho cha kawaida cha sekretariati kilichofanyika mjini Mkambako.Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa,ameshukuru semina iliyotolewa na viongozi wa sekretarieti huku wakiahidi kwenda kutekeleza maelekezo na maagizo ya Chama.
Baadhi ya viongozi wa CCM halmashauri ya mji wa Makambako wakisikiliza semina elekezi ya kikao cha sekretarieti kwa viongozi ili kuwafikishia wanachama wao.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments