Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameendelea kushusha watu kwenye Kikosi chao wakiwemo wataalmu wa Benchi la Ufundi ili kuboresha Kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa mashindano wa 2023-2024.
Watoto wa Msimbazi baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC PL) kwa misimu miwili, sasa wameamua kuboresha Kikosi chao kwa kuweka watu wapya kila idara iliyoonekana kuwa na mapungufu kwao au kuwa na udhaifu.
Baada ya kuachana na baadhi ya wachezaji wake wa kigeni na baadhi ya wachezaji wake wa ndani tena wengine wakongwe kwenye Kikosi hicho, Simba SC wameendelea kutambulisha mbadala wa wachezaji hao waliachwa Kikosini hapo hivi karibuni.
Hadi sasa, Simba SC wamesajili wachezaji wawili ambao tayari imewatambulisha ni Willy Essomba Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda, Aubin Kramo Koume kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast na Mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone kutoka Klabu ya Coton Sports ya Cameroon.
Hata hivyo, Simba SC wamedai wanaendelea kusajili wachezaji wengine zaidi ili kuimarisha Kikosi chao kuelekea msimu ujao wa mashindano wa 2023-2024.
Pia, wamesajili Meneja wa timu na Sayansi ya michezo, Mikael Igendia, Kocha wa Magolikipa, Daniel Cadena (ametoka Azam FC), Mtaalamu wa mazoezi ya viungo (Fitness Coach), Corneille Hategekimana.
Wekundu wa Msimbazi wametajwa kumtoa kwa mkopo Mlinzi wake wa kati, raia wa Kenya, Joash Onyango ambaye picha zake zimeonekana akiwa na jezi ya Singida Fountain Gate FC.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments