RAIS wa wanawake wacheza gofu nchini (TLGU), Queen Siraki, amesema mashindano ya gofu yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya Gymkhana ya ‘Lake Energies’ yameongeza hamasa kwa wachezaji wa mchezo huo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji wa ridhaa, wachezaji wa kulipwa na watoto, Queen alisema ujio wa lake Energies kudhamini mchezo huo umeongeza ushindani kwa wachezaji.
“Mashindano haya yameleta ushindani mkubwa sana na tunatamani lake Energies waendelee kutudhamini kwenye mashindano mengine, tumeshuhudia walimu wetu wanaotufundisha hapa Gymkhana wakishindana wenyewe kwa wenyewe na kutoa somo kwa vijana wengi, kiufupi mashindano haya yamefana sana,” alisema Queen.
Kwa upande wake , Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Energies, Abdirahman Ahmed, alisema kampuni huiyo itaendelea kusapoti mchezo huo na wanafikiria kudhamini mashindano ya ‘Co-operate’ yanayotarajiwa kufanyia mwezi ujao.
“Nawashukuru wote walioshiriki mashindano haya, sisi kama Lake Energies tutaendelea kusapoti michezo kwa sababu tunaamini michezo inaleta umoja na pia ni namna moja wapo ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua michezo nchini,” alisema Ahmed.
Katika mashindano hayo kwa upande wa wachezaji wa kulipwa, Frank Mwinuka aliibuka mshindi wa jumla kwa kupata grosi 71na kukabidhiwa zawadi ya pesa shilingi milioni moja akifuatiwa na Salum Dilunga (grosi 73) ambaye alipata Sh, 664,000 wakati nafasi ya tatu ikishikwa na Rodrick John (grosi 74) na kuzawadiwa Sh. 420,000.

Mbali na fedha hizo, pia washindi walikabidhiwa mitungi ya gesi kutoka kwa kampuni hiyo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments